REKODI YA MKALI WA KUKATA UPEPO, USAIN BOLT YAVUNJWA RASMI….
02:12 | No Comments |
Mwanariadha wa Marekani, Justin Gatlin amevunja rekodi iliyowekwa na Usain Bolt na kuweka rekodi mpya katika mbio za Diamond League za mita 100.
Gatlin mwenye umri wa miaka 33 anayeishi huko Orlando, Florida, aliwaongoza wenzake kushinda kwa sekunde 9.75 ikiwa ni muda bora wa saba kuwekwa katika historia na ameipiku rekodi ya Bolt (lightning Bolt) ya sekunde 9.76 iliyoweka mwaka wa 2012.
Gatlin ambaye amepigwa marufuku kutumia dawa za kusisimua misuli alikimbia mda wa sekunde 9.74 katika mkutano wa kwanza wa mbio za Diamond League mwezi uliopita.
Bingwa wa mbio za Olimpiki Sally Pearson alipata jeraha la kifundo cha mkono baada ya kuanguka katika mbio za kuruka viunzi za mita 100 upande wa wanawake.
0 comments:
Post a Comment