Sunday 17 July 2022

ELIMU..!! JINSI YA KUTUNZA FEDHA YA AKIBA KAMA UNA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA.

Moja ya matatizo yanayowasumbua watu wengi sana ni jinsi ya kutunza fedha ya akiba. Wengi wetu tunapokuwa hatuna hela tunakuwa na mawazo mazuri sana na ukiona mtu anachezea hela unaona kama hana akili au hajielewi. Ila unapozipata hela akili yote inahama, mipango yako yote mizuri unaisahau na unajikuta unatumia tu hovyo mpaka zinaisha. Zikiisha unarudi tena kwenye mzunguko ule wa kupata mawazo mazuri ya kutekeleza utakapopata fedha.

Mambo muhimu ya kufanya ili uepuke matumizi mabaya ya fedha zako.
1. Jijengee nidhamu binafsi. Anza kwa kujipa ahadi ndogo na kisha zitekeleze na uendelee kuongeza ahadi hizo. Usikubali tamaa yoyote ikufanye ushindwe kuheshimu mipango yako.
2. Kuwa na bajeti ya matumizi ya fedha kabla hujapata fedha kama ya mshahara. Kwa kuwa umeshaanza kujijengea nidhamu binafsi weka mipango ya matumizi ya fedha zako na uifuate.
3. Tafuta mtu unayemuamini akuhifadhie fedha zako. Mtu huyu unamwambia kabisa kwamba asikupatie fedha hizo mpaka baada ya muda fulani. Kwa njia hii unaweza kujijengea nidhamu na kuweza kuheshimu maamuzi yako.
4. Angalia aina ya marafiki ulionao au watu unaopendelea kukaa nao. Tabia zako ni wastani wa tabia za watu watano unaopendelea kukaa nao, hivyo kama marafiki zako au watu unaopendelea kukaa nao ni watu wenye matumizi mabaya ya fedha na wewe utakuwa na tabia hiyo. Waangalie vizuri watu unaopendelea kukaa nao na ukiona wana tabia hiyo anza kupunguza muda unaokua nao mpaka kuacha kabisa. Kwa sababu hata ukijijengea nidhamu kama bado utaendelea kuwa karibu na watu hao ni rahisi sana kurudia tabia zako za zamani.
5. Fanya uwekezaji ambao ni vigumu kuchukua fedha zako. Ukiweka fedha benki ni rahisi kuchukua ila kama utaziweka kwenye uwekezaji inakuwa ngumu kidogo kuzichukua. Uwekezaji unaweza kuwa kununua hisa au vipande, kununua viwanja au mali nyingine zisizohamishika kirahisi.
Share na marafiki wapate kujifunza.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA