Thursday, 2 July 2015

GUNDOGAN AITOSA MANCHESTER UNITED NA KUSAIANI MKATABA MPYA BOROSSIA



Ilkay Gundogan ameitosa Manchester United na kusaiani mkataba mpya wa kuitumikia Borossia Dortmund kwa miaka miwili zaidi.
Kwa muda mrefu kiuongo huyo 'fundi' mwenye umri wa miaka 24, alikuwa ana uhusishwa kwa nguvu na uhamisho wa kwenda Manchester United lakini hatimaye amechagua kubaki Dortmund.
Akizungumza baada ya kutangazwa kwa dili lake jipya, Gundogan alisema: "Siku ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya imepita na ni jambo la kuvutia sana kufanya kazi na wachezaji wenzagu pamoja na kocha mpya.
"Nina furaha kubwa kuthibitsha kuwa hatimaye ninaendelea kuichezea Borussia Dortmund." 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA