NATHANIEL CLYNE SASA NI MALI YA LIVERPOOL
Liverpool imekamilisha rasmi usajili wa beki wa Southampton Nathaniel Clyne kwa ada ya pauni milioni 12.5.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano na anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool kiangazi hiki.
Wachezaji wengine waliosajiliwa Liverpool ni kiungo James Milner, mshambuliaji Danny Ings, kiungo mshambuliaji Roberto Firmino, kipa Adam Bogdan na beki Joe Gomez.
Beki wa zamani wa Southampton Clyne amesaini miaka mitano Anfield
Clyne alifuzu vipimo via afya Jumatatu kabla ya kusaini rasmi mkataba wa kuichezea Liverpool
Clyne akitazama mandhari ya jiji la Liverpool
0 comments:
Post a Comment