Saturday, 28 November 2015

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AONGOZA MATEMBEZI KUCHANGIA UNUNUZI WA MADAWATI NCHINI YALIYOANDALIWA NA HASSAN MAJAR TRUST


Mh.Mwinyiakisalimiana na wenyeji wake mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Police Mess kwa ajili ya kuanza matembezi

Mh.Mwinyi akiongoza mamia ya watembeaji kufanya mazoezi kabla ya kuanza matembezi

 Na Dickson Mulashani 

Leo, Rais mstaafu wa awamu ya pili Mh.Ali Hassan Mwinyi ameongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam katika matembezi maalum yaliyoandaliwa na Hassan Majar Trust kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati ili kupunguza tatizo la wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini.

Balozi wa matembezi hayo MSanii Mwasiti akijiweka tayari kabla ya kuanza matembezi

Brass band ya Jeshi la polisi likiongoza matembezi






Askari wa barabarani akiwahi mbele ya msafara ili kuhakikisha njia ipo salama
Baadhi ya wapiga picha katika mikao mbalimbali ili kupata picha



Mh.Mwinyi akitoa salamu za shukrani kwa wadau walifika

Akitoa salamu kwa waliofika na kushiriki matembezi hayo,Mzee Mwinyi aliwashukuru waandaji wa mpango huu na kutoa wito kwa Watanzania kujinyima na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili wachangie elimu.

Bi Zena Tenga akitoa salamu za shukrani mara baada ya matembezi
Kwa mujibu wa mwaandaji wa matembezi hayo Bi Zena Tenga, amesema Hassan Maraj Trust kama mdau wa elimu inasikitishwa sana na hali ya wanafunzi kusoma katika mazringira yasiyo rafiki na kupelekea elimu ya taifa letu kushuka.


Katika maelezo yake Bi Zena aliwashukuru wadau waliojitokeza kushiriki na kuchangia matembezi hayo na kubainisha kuwa hadi sasa zaidi ya madawati 8,000 yameshapatikana na tayari wanafunzi zaidi ya 24,000 wameinuliwa toka sakafuni na kusoma kwa utulivu.
Mmoja kati ya waandaji wa matebezi hayo akisema jambo wakati wa utambulisho
Baadhi ya wazee ambao ni wadau wa mfuko huo

Wadau kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushiriki matembezi hayo


0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA