ANDY CAROLL APIGA HAT-TRICK NA KUZIDI KUITIBULIA ARSENAL MAHESABU YA UBINGWA
Magoli matatu ya Andy Caroll kwa lugha ya soka hat-trick yameleta pigo kwa timu ya Arsenal ambayo tayari inanafasi finyu ya matumaini ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza licha ya washika mtutu hao kulazimisha sare ya mabao 3-3 dhidi ya West Ham.
Arsenal ambayo ipo pointi 10 nyuma ya vinara wa Leicester City ikiwa na michezo sita iliyobakia, ilipata bao la kwanza kupitia kwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez kuongeza la pili baada ya kupatiwa pande na Alex Iwobi na kuongoza kwa mabao 2-0.
Hata hivyo Andy Caroll alipachika mabao mara mbili ndani ya sekunde 160, na kuifanya West Ham kusawazisha, na kisha baadaye katika kipindi cha pili alipiga kichwa kilichoingia kwenye posti na kuandika bao la tatu kabla ya Laurent Koscielny kuisawazisha Arsenal. Andy Caroll akiwa kazini, hakika leo alikuwa mwiba mkali dhidi ya Arsenal Alexis Sanchez akimshukuru alex Iwobi kwa kumpa pande lililozaa bao la pili kwa Arsenal

0 comments:
Post a Comment