Thursday 7 April 2016

MANCHESTER CITY YAJIKAKAMUA NYUMBANI KWA PSG

Goli la Fernadinho limeiwezesha Manchester City kupata sare muhimu ugenini katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris St-Germain ulioishia kwa sare ya mabao 2-2.

Katika mchezo huo Kevin de Bruyne alimalizia vizuri mpira na kuipatia Manchester City bao la kuongoza baada ya Joe Hart kuokoa penati iliyopigwa na Zlatan Ibrahimovic.

Hata hivyo Ibrahimovic alitumia vyema makosa ya Fernando na kusawazisha bao hilo na baadaye Adrien Rabiot kutumbukiza la pili baada ya mapumziko na kuifanya PSG kuongoza.
                                            Kevin de Bruyne akipachika bao kwa shuti kali
             Zlatan Ibrahimovic akiwa amepachika bao huku Joe Hart akihamaki
                                Angel Di Maria akipaa baada ya kukwatuliwa na Mangala

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA