Sunday 17 April 2016

SAMATTA AENEDELEA KUTUPIA KRC GENK IKISHINDA 2-1

Mbwana Samatta  akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la kwanza

NYOTA ya Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta imeendelea kung’ara Ulaya baada ya leo kuifungia tena klabu yake, KRC Genk katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji uliofanyika Uwanja wa Regenboogstadion mjini Waregem, Samatta alifunga bao la kwanza dakika ya saba tu kwa kichwa akimalizia krosi ya mkongwe wa umri wa miaka 25, Mbelgiji Thomas Buffel.

Beki wa Kongo mzaliwa wa Ufaransa, Marvin Baudry akajifunga katika harakati za kuokoa dakika ya 15 kuipatia Genk bao la pili, kabla ya mshambuliaji Msenegali, M'Baye Leye kuifungia SV Zulte-Waregem bao la kufutia machozi kwa penalti dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza.

Hilo linakuwa bao la nne kwa Samatta katika mechi tisa alizocheza tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC. 
Mabao mengine alifunga katika ushindi wa 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA