Sunday 17 April 2016

SERGIO AGUERO AIZAMISHA CHELSEA DARAJANI KWA KUFUNGA HAT-TRICK


Mshambuliaji hatari Sergio Aguero amefunga mabao matatu yaani hat-trick na kuipa ushindi Manchester City unaoifanya kukaribia kujihakikishia kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Chelsea magoli 3-0.

Manchester City ilipata goli lake la kwanza baada ya Aguero kupata pasi kutoka kwa Kevin De Bruyne, na kisha De Bruyne tena akafanya shambulizi na kumpa pande Samir Nasri aliyemlisha Aguero na kuandika goli la pili. Aguero, alifunga la tatu kwa mkwaju wa penati.
                                Sergio Aguero akipiga shuti lililojaa langoni mwa Chelsea
                        Kipa wa Chelsea Courtois akionyeshwa kadi nyekundu na refa

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA