Monday, 30 May 2016

HOJA YA WANAFUNZI 7000 WALIOFUKUZWA UDOM YACHAFUA HALI YA HEWA DODOMA, BUNGE LAAHIRISHWA HADI SAA KUMI


 Naibu Spika wa Bunge ameahirisha Bunge kabla ya muda wake baada ya wabunge kutaka kujadiliwa suala la wanafunzi wa UDOM kufukuzwa chuoni wakati hawana kosa.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari aliomba mwongozo na kutaka sakata la wanafunzi hao lijadiliwe lakini Naibu Spika, Tulia Ackson alisema jambo hilo haliwezi kusitisha shughuli za Bunge hivyo haliwezi kujadiliwa kwa wakati huo.
Wabunge wakiondoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Naibu Spika kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge leo.

Kauli hiyo iliwanyanyua wabunge wa upinzani na baadhi ya wa CCM wakipinga kauli hiyo huku wakiwa wamesimama jambo ambalo lilisababisha kuaihirishwa kwa Bunge hadi saa 10:00 jioni huku akiagiza kukutana kwa kamati ya uongozi ya Bunge.
Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge Mbunge wa jimbo la Mwibara (CCM) Mheshimiwa Kangi Lugoja amesema hakubaliani na maamuzi ya naibu spika kukataa suala hilo nyeti lisijadiliwe akieleza kuwa binafsi ameshuhudIa baadhi ya wanafunzi waliofukuzwa wakiwa katika hali ya sintofahamu.

 "Binafsi jana nimewapa lifti baadhi ya wanafunzi wanasanduku na mabegi wanalia hawana namna ya kufanya, mimi kama mbunge wa CCM muongozo ulioombwa hapa ndani na mbunge wa upinzani Mheshimiwa Joshua Nassari kwamba tuahirishe shughuli zilizoorodheshwa leo ili tujadili jambo muhimu linalohusu nchi yetu , maamuzi yaliyotolewa na  naibu spika mimi sikubaliani nayo ni maamuzi ambayo yanazidi kuwavuruga watoto wengine hatujui usalama wao leo wamelala vipi .kwahiyo mimi kama mbunge wa CCM ninachohitaji lazima shughuli nyingine zisimame ili tujadili suala hili".

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA