LIVERPOOL YATANGAZA KUMUWINDA BEKI HUMMELS WA DORTMUND
KLABU ya Liverpool imeingia
katika vita ya kumwania beki mahiri wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, Mats
Hummels. Habari zinasema kwamba kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ameamua
kuingia katika vita ya kumwania beki huyo kutokana na ukweli kwamba beki huyo
sasa hana mapenzi tena ya kucheza katika klabu hiyo ya zamani ya mwalimu huyo.
Klopp amekaririwa akisema kwamba
anataka kumsajili beki huyo kutokana na mahitaji ya sasa ya beki wa aina yake
na kwamba haoni kama ni lazima beki huyo kwenda katika timu pinzani ya Bayern
Munich. “Ni kweli kwamba mchezaji huyo ameonekana anataka kwenda Bayern lakini
mimi pia nataka kuzungumza nae na kumsajili hapa Liverpool,” amesema Klopp.
Mapema wiki iliyopita beki huyo ameiambia klabu yake kuwa anataka kujiunga na
viongozi wa Ligi ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, Bayern Munich baada ya
kukamilika msimu huu.
Mats Hummels amesema hana amani
katika kikosi hicho na kwamba anataka kukatiza mkataba na kuangalia maisha
mengine. Mapema wiki hii, mwenyekiti wa Bayern, Karl Heinz Rummenigge alifichua
kuwa klabu hiyo ilikuwa tayari inafanya mazungumzo na nahodha huyo wa Dortimund
kuhusu uhamisho.
Dortmund imethibitisha katika taarifa kuwa
mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani mwenye umri wa miaka 27 ambaye ana
mkataba hadi Juni, 2017 amewasilisha ombi rasmi la kutaka kuondoka. Kwa sasa
Bayern haijatoa ofa na kuwa mchezaji huyo ataweza kuondoka tu ikiwa kwa
kutolewa kiasi cha pesa kitakachokubaliwa.
Hummels atajiunga na Mario Goetze aliyeondoka
mwaka 2013 kwa kiasi cha euro milioni 37 na mshambuliaji Robert Lewandoswki
aliyesaini mwaka 2014. Hata hivyo, kocha wa Liverpool amesema ni wakati mwafaka
sasa kumsajili mchezaji huyo aisema kwamba yuko katika orodha ya wachezaji
ambao anawataka kutoka Borussia alikotokea kabla ya kujiunga na Liverpool.
0 comments:
Post a Comment