EURO 2016:: ITALIA YAILIZA UBELIGIJI ,SWEDEN ,IRELAND HAKUNA MBABE
Emanuele Giaccherini akiiandikia Italia bao la kwanza ikiwa ni goli lake la kwanza kufunga akiichezea timu ya taifa |
ITALIA imeianza vyema michuano ya Euro baada ya kuichapa Ubelgiji magoli 2-0 katika uwanja wa Stade's de Lumiere's katika mchezo wa kwanza wa kundi E.
Emanuele Giaccherin ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwafungia Italia goli la kwanza dakika ys 32 baada ya kupokea pasi toka kwa Leornado Bonucci upande wa kulia.
Ubelgiji walikuja juu baada ya goli hilo lakini ukuta wa Italia uliokuwa chini ya Giorgio Chielini, Bonucci na Barzagli ulikuwa makini kuondoa hatari toka kwa kikosi chenye mastaa kibao akiwemo Eden Hazard, Lukaku, Origi pamoja nyota wengine.
Kocha wa Italia Antonio Conte alipatwa na hali ya kuvuja damu puani wakati akishangilia goli la kwanza |
Pelle akiachia shuti lililojaa wavuni na kuiandikia Italia bao la pili |
Huku watu wakiamini mchezo huo ungeisha kwa ushindi wa goli moja Graziano Pelle aliipatia goli la pili Italia dakika za nyongeza na kuwafanya kuibuka na ushindani wa magoli 2-0.
Kevin De Bruyne akichauana na beki Matteo Darmian (kulia) wakati wa mchezo |
Sasa Ubelgiji watalazimika kushinda na kutoa sare michezo miwili iliyosalia ili kujiweka katika nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Italia wanaongoza kundi E wakiwa na alama tatu wakifutiwa na Ireland na Sweden waliotoka sare ya goli 1-1.
Nyota wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic akipongezana na wachezaji wenzake, John Guidetti na Kim Kallstrom baada ya timu yao kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Ciaran-Clarkis aliyejifunga katika sare ya 1-1, kufuatia Wes Hoolahan kuanza kuifungia Jamhuri ya Ireland Uwanja wa Stade de France mjini Paris, Ufaransa katika mchezo wa Kundi E Euro 2016
0 comments:
Post a Comment