Saturday 11 June 2016

TAREHE YA MWISHO YA KULIPA KODI YA MAPATO NA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT)


Walipakodi wote wanakumbushwa kuzingatia mwisho wa kulipa kodi ya Mapato na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) PASIPO ADHABU

1.O    ULIPAJI WA KODI YA MAPATO – MAKADIRIO YA AWALI

⦁    walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/06/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya nne ya makadirio ya awali ya mwaka 2016
⦁    walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/09/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya tatu ya makadirio ya awali ya mwaka 2016
⦁    walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/12/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya pili
⦁    walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 31/03/2017, wanapaswa kulipa sehemu ya kwanza ya makadirio ya awali ya mwaka 2017
 
Tarehe za malipo kwa ufupi:
Tarehe ya mwisho wa mwaka wa Mahesabu    Awamu za Malipo    Tarehe ya Mwisho wa Malipo bila Adhabu
30/06/2016    Awamu ya nne ya mwaka wa Mapato 2016    30/06/2016
30/09/2016    Awamu ya tatu ya mwaka wa Mapato 2016    30/06/2016
31/12/2016    Awamu ya piliya mwaka wa Mapato 2016    30/06/2016
31/03/2017    Awamu ya kwanza ya mwaka wa Mapato 2017    30/06/2016

2.0    UWASILISHAJI WA RITANI ZA MAPATO KWA MWAKA 2016
Walipakodi wote ambao mwaka wao wa mapato uliisha tarehe 31/12/2015, wanatakiwa kuwasilisha ritani zao pamoja na hesabu zilizokaguliwa na kulipa kodi yote inayotakiwa mnamo au kabla ya tarehe 30/06/2016

3.0    UWASILISHAJI WA RITANI ZA VAT ZA MWEZI MEI 2016
Walipakodi wote ambao wamesajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wanatakiwa kuwasilisha ritani za mwezi mei 2016 na kulipa kodi inayotakiwa kabla ya tarehe 30/06/2016. Pia wale wote ambao hawakufanya biashara wanatakiwa kuwasilisha ritani zao zisizokuwa na malipo (NIL RETURN)

4.0    UTOAJI WA RISITI ZA KODI ZA KIELEKITRONIKI/ ANKARA YA KODI
Walipakodi wote waliosajiliwa na wasiosajiliwa kwenye kodi ya Ongezeko la Thamani wanakumbushwa Kutoa risiti za kodi za kielekitroniki/Ankara ya kodi kwa mauzo yote wanayofanya kulingana na fedha zilizopokelewa. Ni kinyume cha sheria kupokea malipo kwa kuuza Bidhaa au huduma bila Kutoa risiti ya kodi ya kielekitroniki/Ankara ya kodi

5.0    KUMBUKA
Riba na Adhabu itatozwa/itatolewa kwa Pointi ya Sarafu (Currency Points) kwa mlipakodi yeyote ambaye hatalipa kodi kwa muda unaotakiwa au atakayeshindwa kuwasilisha ritani kwa muda unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Ili kuepuka  msongamano na usumbufu mwingine walipakodi wanashauriwa kutosubiri siku ya Mwisho. Tunashukuru kwa ushirikiano mzuri.

“Pamoja Tunajenga taifa letu”

Imetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa mlipakodi
TRA Makao Makuu
S.L.P 11491
Dar es Salaam.

    Barua pepe:     huduma@tra.go.tz
Kituo cha Huduma
Simu bila Malipo
0800 780078
0800 750075

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA