Friday 22 July 2016

USAJILI MAJUU:: WIJNALDUM ATUA LIVERPOOL AKITOKEA NEWCASTLE UNITED


Katika kile kinachoonekana kuwa kocha wa Liverpool inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza ,Klopp kujenga kikosi kikubwa na tishio ili kurejesha makali ya mabingwa hao wa kihistoria barani Ulaya, Liverpool imefanikiwa kumnasa mchezaji mahiri na machachari Georginio Wijnaldum toka  timu ya Newcastle United kwa ada ya pauni milioni 25 ambapo atavaa jezi namba tano.
 
Katika siku za karibuni Wijnaldum alikuwa akihusishwa na vijogoo hao wenye maskani yao jijini Liverpool na hatimaye tayari amekuwa mmoja wa wanafamilia hiyo.Wijnaldum aliyetua Uingereza msimu uliopita akitokea PSV Eindhove alijikuta akianza vyema na kuizoea ligi hiyo mashuhuri na kufanikiwa kuwa mfungaji bora katika timu ya Newcastle kwa kupachika mabao 11 katika michezo 38.

Katika uhamisho huu inasemekana licha ya kuwa Newcastle kushuka daraja ndio chanzo, lakini uhusiano kati ya kocha wa sasa Newcastle Rafa Benitez dhidi ya timu yake ya zamani Liverpool umekuwa sababu muhimu ya kukamilika.

"Binasfi nina msisimko kwasababu Liverpool ni klabu kubwa yenye historia kubwa na mara nyingi ni ndoto ya kila mchezaji kucheza kwenye  klabu kubwa kama Liverpool" Wijnaldum aliuambia mtandao wa Liverpoofc.com mara baada ya kutia saini.

 
Ni dhahiri kuwa kwa sasa mchezaji huyu ambaye amekuwa wa sita kusajiliwa msimu huu na anaiongezea Liverpool uwanja mpana wa uchaguzi katika nafasi za kiungo mshambuliaji na atalazimika kusafiri kuelekea nchini Marekani ambapo Liverpool imeweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.
 PICHA ZOTE NA Liverpoolfc.com

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA