WAMEAMKA::ARSENAL YAIBUKIA KWA WATFORD
Arsenal imecharuka na kuifunga nyumbani Watford kwa magoli 3-1 ikiwa ni ushindi wao wa kwanza katika msimu huu.
Katika mchezo huo Santi Cazorla alikuwa wa kwanza kuifungia Arsenal goli la kwanza na kisha Alexis Sanchez kuongeza la pili na Mesut Ozil kufunga la tatu kabla ya mapumziko.
Watford ilijitutumua katika kipindi cha pili na kupata goli manomo dakika ya 56 kupitia mpira wa guu la kushoto la Roberto Pereyra.
Santi Cazorla akipiga mpira wa penati na kuifungia Arsenal goli la kwanza
Mpira uliopigwa na Alexis Sanchez aliyeanguka chini pembeni ya goli ukiingia wavuni na kuandika goli la pili.
0 comments:
Post a Comment