Wednesday 28 September 2016

UEFA:: SON HEUNG-MIN AENDELEA KUONESHA MAKALI YAKE SPURS IKISHINDA 1-0


Mshambuliaji Son Heung-min ameendelea kuonyesha kiwango chake na kuipatia Tottenham ushindi wa kwanza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi.

Mchezaji huyo raia wa Korea Kusini alifunga goli lake la tano katika michezo mitano, kwa kutumbukiza wavuni pasi ya Erik Lamela na kufanya matokeo kuwa 1-0.

Tottenham walioonekana kutokuwa vizuri katika mchezo wao wa awali dhidi ya Monaco, walionekana vizuri Urusi na kutandaza soka safi.
Son Heung-min akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli pekee katika mchezo huo
                      Mchezaji wa Tottenham Dele Alli akichuana na beki CSKA Moscow

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA