Monday 21 November 2016

COSTA AIWEKA CHELSEA KILELENI MWA LIGI KUU YA UINGEREZA

Goli la kumi la Diego Costa katika msimu huu limeiwezesha Chelsea kukwea kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza na kuizamisha Middlesbrough katika dimba la Riverside kwa ushindi wa goli 1-0.

Chelsea ambayo hadi sasa haijapoteza michezo sita mfululizo ilianza kwa kasi katika mchezo huo mgumu na kufanikiwa kufunga goli pekee katika dakika ya 41.

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema anashindwa kuamini ni kwa jinsi gani mabadiliko yanotoendelea katika timu yake yalivyopelekea kuongoza ligi.
 Shuti lililopigwa na Diego Costa kati kati ya msitu wa mabeki likimshinda kipa na kuelekea wavuni
         Kipa wa Middlesbrough akifanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliopigwa na Pedro

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA