Wednesday 30 November 2016

KLOPP ASEMA PENGO LA COUTINHO HALITAIKWAMISHA LIVERPOOL


KOCHA mkuu wa timu ya Liverpool mjerumani Jurgen Klopp amesema timu yake inaweza kukabiliana na wapinzani bila ya kuwepo kiungo fundi raia wa Brazil Phillipe Coutinho baada ya nyota huyo  kupata majeraha katika mechi dhidi ya Sunderland wikiendi iliyopita.


Kiungo huyo  alianza vizuri msimu wa 2016/17 kwa kufunga magoli matano katika mechi 13 mpaka sasa lakini Klopp bado anaamini wataibuka na ushindi katika michezo ijayo huku hili likijidhihirisha katika mchezo wa Capital One dhidi ya Leeds United katika dimba la Anfield baada ya Liverpoolkuibuka na ushindi wa magoli mawili.

Klopp alisema "naweza sema hakuna kisingizio chochote kwa sasa, pamoja na uzuri wa Coutinho ila hawezi badili matokeo peke yake uwanjani ila 
kila mtu anahitaji kupigania  timu".

Coutinho anategemea kuwa nje ya uwanja kwa wiki tano hadi sita.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA