Thursday 1 December 2016

EFL CUP::MANCHESTER UNITED YATINGA NUSU FAINALI, SOUTHAMPTON YAIONDOSHA ARSENAL

Manchester United 4-1 West Ham: Anthony Martial and Zlatan Ibrahimovic send Red DevilsTIMU ya Manchester United imeungana na Liverpool, Hull City pamoja na Southampton katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la ligi baada ya kuifunga West Ham United mabao 4-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.

United waliingia uwanjani kwa nguvu kwenye mchezo huo wa kombe la FA ambapo dakika ya pili Zlatan Ibrahimovic ilifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya Henrik Mikhtaryan.

Anthony Martial alifunga mabao mawili kabla ya Ibrahimovic kufunga la mwisho dakika za majeruhi na kuhitimisha karamu hiyo ya magoli. Bao la wageni lilifungwa na Ashley Fletcher akimalizia kazi nzuri ya Dimitry Payet.

Wikiendi iliyopita timu hizo zilikutana uwanjani hapo kwenye mchezo wa ligi kuu na kwenda sare ya bao 1-1 licha ya wenyeji kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

Arsenal 0-2 Southampton: Jordy Clasie and Ryan Bertrand send the Saints into EFL Cup
Wachezaji wa Southampton wakishangilia bao dhidi ya Arsenal katika mchezo wa robo fainali uliopigwa katika dimba la Emirate
Mchezo mwingine Arsenal imetolewa kwenye mashindano hayo baada ya kukubali kichapo nyumbani cha mabao 2-0 toka kwa Southampton.

Michezo ya nusu fainali itachezwa Januari 9 ambapo United itawakaribisha Hull City huku Southampton ikimenyana na Liverpool. Mechi za marudio zitapigwa Januari 23.

-photo credit SPORTMAIL

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA