(USAID) YAWAKWAMUA AKINA MAMA WAJASIRIAMALI WILAYA YA MBOZI MKOANI SONGWE
Akina mama wajasiriamali wa Wilaya ya Mbozi wakiandamana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani
Na Tadeo Jackson
Mradi wa nafaka unaofadhiliwa na shirika la kimarekani (USAID)ambao unajukumu la kuboresha mifumo ya masoko kwa sekta binafsi umeweza kufika katika kijiji Isansa wilaya ya Mbozi mkoani Songwe kwa lengo la kuwahamasisha na kuwapa elimu wanawake ambao wamejikita katika shughuli za ujasiriamali.
Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, mradi wa nafaka ulitoa
elimu kwa wananchi wa Isansa kuunda vikundi ili kuweza kupata msaada wa kielimu
juu ya utunzaji wa mazao mbalimbali wanayolima.
Ikiwa ni mojawapo ya
malengo ya mradi wa nafaka
hasa katika kuboresha ushindani na kuongeza tija, faida na lishe bora kwa walengwa kupitia uboreshaji wa mifumo ya usambazaji
pembejeo, pia umairishaji wa taasisi na
rasilimali watu na uboreshaji wa kusindika mahindi na mpunga.
Mkazi wa Wilaya ya Mbozi kijiji cha Isansa Magdalena Edward Haule akielezea namna alivyofaidika na Mradi unaofadhiliwa na (USAID)
Magdalena Edward Haule ni miongoni mwa akina mama kutoka katika kijiji cha Isansa ambaye amepata faida kubwa kutoka katika mradi wa nafaka baada ya kupata mafunzo juu ya utumiaji wa pembejeo za kilimo na namna anavyotakiwa kutunza mazao bila kuharibiwa na wadudu waharibifu wa mazao.
Magdalena Edward Haule ni miongoni mwa akina mama kutoka katika kijiji cha Isansa ambaye amepata faida kubwa kutoka katika mradi wa nafaka baada ya kupata mafunzo juu ya utumiaji wa pembejeo za kilimo na namna anavyotakiwa kutunza mazao bila kuharibiwa na wadudu waharibifu wa mazao.
Bi haule
amesema alijiunga na mradi wa nafaka tangu mwaka 2015 na kuanzia mwaka
huo na kupata mafunzo mengi ambayo yameendelea kumsaidia yeye na kikundi walichokiunda kwa minajili ya
kupata misaada ya kielimu kutoka Mradi
wa Nafaka.
Na miongoni mwa mafunzo aliyoyapata mama huyu ni pamoja na matumizi mazuri ya mbolea, namna ya kupanda, kuvuna,
kupukuchua mahindi na namna ya kuifadhi
mazao baada ya kuyavuna kutoka shambani.
Pamoja na hayo Bi Haule ametaja faida ambazo wamezipata kupitia mradi
wa nafaka hasa katika utunzaji wa
pamoja wa mazao kama kikundi na
kuweza kuuza kwa pamoja, pia faida
nyingine alizopata ni pamoja na jinsi ya kutunza mazao bila kuharibika kwa muda
mrefu.
Naye Mratibu wa nafaka katika Wilaya ya Mbozi Ibrahimu Mkwiru amekuwa katika mstari mbele katika kuwaelimisha wakulima wa vijiji mbalimbali katika wilaya
ya mbozi ili waweze kupata maendeleo
kupitia shughuli mbalimbali za kiujasiriamaki ikiwa ni pamoja na kilimo na
kuwamasisha wanawake waweze kujishughulisha kuliko kumtegemea mwanaume kwa kila
kitu.
Mratibu wa nafaka katika Wilaya ya Mbozi Ibrahimu Mkwiru akiongea na wajasiriamali waliofika katika maadhimisho hayo
Bwana Mkwiru alisema
kuwa Mradi wa Nafaka umewalenga wakulima hasa vijana na wanawake katika kuwanyeyua
na kuwashirikisha katika kuwapa
elimu mpya ya kiteknolojia hasa ukulima.
Mpunga na mahindi ni
mazao muhimu ya chakula yanayozalishwa
na wakulima wadogowadogo nchini Tanzania pia Mradi wa Nafaka unalenga
kuendeleza shughuli za awamu ya
kwanza ya Mradi wa Nafaka ambao
ulibuni mifumo bora ya kiteknolojia
inayoweza kuigwa katika sehemu na nyanya mbalimbali.
Shughuli za Nafaka pia
zinalenga kuendeleza mafanikio ya kazi
ya Mradi wa (USAID), Tuboreshe chakula
ambao uliendeleza kishe jwa njia ya kurutubisha vyakula
kwa kuongeza viini lishe na
kuboresha usindikaji wa mazao na kusababisha ongezeko la
uhitaji wa unga na mahindi wenye viini lishe.
0 comments:
Post a Comment