Monday 18 April 2016

ARSENAL YAKAMATIWA CHINI NA CRYSTAL PALACE

Mchezaji Yannick Bolasie ametumia shambulizi la dakika za mwisho kuipatia Crystal Palace goli lililoipa sare ya 1-1 dhidi ya Arsenal katika mchezo ambao Arsenal iliutawala.

Arsenal ingeweza kushinda kiurahisi na kukwea juu ya Manchester City na kuitwaa nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi lakini imejikuta ikibakia katika nafasi ya nne.

Katika mchezo huo Alexis Sanchez alifunga kwa mpira wa kichwa akiunganisha pande la Danny Welbeck, na kuwafanya the Gunners kuongoza.

                                  Alexis Sanchez akipiga kichwa cha aina yake kilichojaa wavuni

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA