Sunday 17 April 2016

LEICESTER CITY CHUPUCHUPU KUZAMA KWA WEST HAM


Penati ya dakika ya mwisho wa mchezo iliyopigwa na Leonardo Ulloa, imeisaidia Leicester City iliyobakia na wachezaji kumi dimbani kupata pointi moja dhidi ya West Ham iliyokuwa ikitishia kutibua mahesabu yao ya kuelekea kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza.

Goli la kwanza lililofungwa na Jamie Vardy katika kipindi cha kwanza liliwafanya wenyeji Leicester City kuongoza, na baadaye Vardy alipewa kadi ya njano ya katika dakika ya 56 kwa kujirushwa kwenye eneo la penati na kulazimika kutolewa nje.

Alikuwa Andy Carroll aliyesawazisha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 84 na kisha baadaye Aaron Cresswell kufunga goli safi katika dakika ya 86, hata hivyo penati ya Ulloa ilifanya mchezo kuisha kwa sare ya mabao 2-2.
                                     Jamie Vardy akipachika bao la kwanza la Leicester City
                Jamie Vardy akimbwatukia refa baada ya kumpa kadi ya pili ya njano

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA