Wednesday 6 April 2016

UEFA::SUAREZ AITETEA BARCELONA ,TORRES AKILIMWA KADI NYEKUNDU


MABINGWA wa zamani wa Ulaya, Barcelona ya Hispania na Bayern Munich ya Ujerumani, zote zimepata ushindi mwembamba katika mechi zao za kwanza za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa nyumbani.
Barcelona imewafunga washiriki wenzao wa La Liga ya Hispania, Atletico Madrid mabao 2-1 Uwanja wa Camp Nou.
The Atletico Madrid No 9 wheels away in celebration following his opening goal against La Liga rivals Barcelona on Tuesday night
mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea za England, Fernando Torres alianza kuifungia  Atletico Madrid dakika ya 25, kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakika 10 baadaye kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano..
Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez (kulia) akishangilia baada ya kuifungia timu yake usiku huu

Luis Suarez akaisawazishia Barca dakika ya 63 na kuifungia bao la ushindi dakika ya 74.
Matokeo hayo, yanamaanisha Barca bado haipo salama, kwani inaweza kutolewa iwapo itafungwa 1-0 katika mchezo wa marudiano mjini Madrid.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA