Friday 21 October 2016

EUROPA CUP::POGBA APIGA 2 MAN UNITED IKITAKATA 4:1 DHIDI YA FENERBAHCE


Kiungo ghali zaidi aliyesajiliwa na Manchester United msimu huu akitokea Juventus ,Paul Pogba amekonga nyoyo za mashabiki wa timu hiyo alipopachika mabao mawili kati ya manne yaliyoipa ushindi Manchester United dhidi ya klabu ya Fenerbahce katika michuano ya Europa uliopigwa katika uwanja wa Old Trafford jana usiku.
Manchester United ilipata mabao matatu ya utangulizi katika kipindi cha kwanza huku mawili kati yao yakiwa kwa mikwaju ya penat ambapo moja lilifungwa na Pogba huku Martial akifunga jingine kabla ya Pogba kufunga tena kwa shuti toka nje ya kumi na nane.

Sambamba na hilo mshambuliaji Robin Van Persie nae aliipatia Fenerbahce bao la kufutia machozi dhidi ya timu yake ya zamani na mchezo kumalizika kwa United kushinda bao 4: 1 kufuatia Jesse Lingard kupachika bao la nne katika dakika ya 48 kipindi cha pili

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA