Showing posts with label AJIRA. Show all posts
Showing posts with label AJIRA. Show all posts

Saturday, 10 December 2016

MAJALIWA ATOA TUZO YA MWAJIRI BORA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa tuzo ya mwajiri bora kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akizungumza kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kukabidhi tuzo kwa washindi wa tuzo ya mwajiri bora kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo ya mshindi wa Jumla ya Mwajiri Bora, Bw. David Magese wa Kampuni ya Bia Tanzania baada ya kampuni yake kunyakua tuzo hiyo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kiataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo ya mshindi wa Jumla ya Mwajiri Bora, Bw. David Magese wa Kampuni ya Bia Tanzania baada ya kampuni yake kunyakua tuzo hiyo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kiataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo ya mwajiri bora kwenye Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na wapili kulia kwake ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Posi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Saturday, 3 December 2016

TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAMKO KUFUATIA UTUMBUAJI NA TUHUMA ZA KUWADHALILISHA WATUMISHI WA UMMA


Tume ya Utumishi wa Umma imetaja mamlaka sita zenye dhamana na madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma kisheria ikiwa pamoja na kufuta nafasi za madaraka. 

Vilevile, Tume hiyo imezitaka mamlaka za nidhamu zote kuzingatia sheria, kanuni pamoja na taratibu wakati wa kutekeleza majukumu yao kwani kwa kufanya hivyo, watumishi wanaotuhumiwa kufanya kosa watatendewa haki. 

Tume ya Utumishi wa Umma imetoa maelekezo hayo siku chache baada ya viongozi wengi katika Serikali ya Awamu ya Tano wakiwamo wakuu wa mikoa na wilaya kuwachukulia kiholela hatua za nidhamu watumishi wa umma wakati baadhi hawana mamlaka hayo kisheria. 

Baadhi ya wakuu wa mikoa wamekuwa waki- wasimamisha watumishi hadharani tena kwa kusikiliza malalamiko ya upande mmoja bila kuwapa walalamikiwa nafasi ya kujitetea, na wakati mwingine kudhalilishwa katika mikutano. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Msaidizi Tume hiyo, Enos Mtuso alisema kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma yako chini ya watu wachache. 

“Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 ilitungwa ili kuweka misingi ya kisheria katika kutekeleza malengo ya Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma iliyopitishwa na Serikali mwaka 1998. 

Sheria hii ndiyo inayotoa uwezo kwa mamlaka za kinidhamu mbalimbali katika utumishi wa umma na kuweka misingi ya namna masuala hayo yanavyopaswa kushughuliwa,” alisema. 

Mtuso alizitaja mamlaka hizo kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Katibu Mkuu Kiongozi, watendaji wakuu, wakuu wa idara na divisheni, na mamlaka za Serikali za Mitaa (Baraza la Madiwani). 

Lakini alipoulizwa mkuu wa mkoa anapata wapi mamlaka ya kuwafukuza kazi watumishi wa umma na kuwadhalilisha mbele ya hadhara, Mtuso alisema wao kama Tume hawana mamlaka ya kuzungumzia jambo hilo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanakiuka maadili na kwamba suala hilo liko chini ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. 

Kauli ya Tume iliwekewa uzito na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jaffo ambaye amewataka wakuu wa idara kuacha kuwanyanyasa wafanyakazi kwani hali hiyo inasababisha wafanye kazi kwa hofu ya kutumbuliwa. 

Akizungumza baada ya kuwatembelea watumishi wa umma wa Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam jana, Jaffo alisema wizara yake itatoa ushirikiano kwa watumishi wote wanaofanya kazi kwa bidii. 

Katika hatua nyingine, Mtuso alitoa takwimu za mashauri ya nidhamu yaliyochukuliwa hatua katika kipindi cha 2014/2015 na 2015/2016 akisema jumla ya watumishi wa umma 249 sawa na asilimia 75 ya mashauri yote yaliyowafikia wakiwamo walimu 209 walifukuzwa kazi kwa makosa yaliyothibitika.

 Alisema Watumishi hao wamefukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwamo, kukiuka maadili ya kazi, kutotekeleza majukumu, ubadhilifu, rushwa, wizi wa fedha na mali, udanganyifu, matumizi mabaya ya madaraka, uzembe, utovu wa nidhamu huku utoro kazini ukiwa na idadi kubwa ya waliofukuzwa kazi. 

“Utoro kazini ni changamoto kubwa inayotukabili na ndiyo mashauri yake mengi yanathibitika, unakuta mtumishi haendi kazini siku tano na kuendelea bila sababu maalumu wala hatoi taarifa yoyote kwa waajiri wake kuwa anashida gani,” alieleza.

Tuesday, 25 October 2016

SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUWA ITAANZA KUTOA AJIRA


1.Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira, kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi Februari, 2017. Chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye kusambazwa katika mitandao mingine.

2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha

Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.


3.Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka husika.

5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali. 
Imetolewa na:

Tuesday, 30 August 2016

SERIKALI YABAINISHA ITATOA AJIRA MPYA 71,496

SERIKALI imeanza kuwashughulikia watumishi walionufaika na fedha za watumishi hewa ambapo hadi sasa watumishi 839 wapo katika hatua mbalimbali wakiwemo waliofikishwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wengine wanaendelea kuhojiwa polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.

Sambamba na hilo, serikali inatarajia kutoa ajira mpya 71,496 kwa mwaka huu wa fedha baada ya kukamilisha uondoaji wa wafanyakazi hewa. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki aliyasema hayo wakati akizungumzia utekelezaji wa mipango na mikakati ya wizara yake katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1). Kairuki alisema,

“Kwa sasa tayari wapo watumishi wameshahojiwa na kuchukuliwa maelezo yao polisi na upelelezi utakapokamilika watachukuliwa hatua mbalimbali za kisheria, ikiwemo kufikishwa mahakamani… Tunakamilisha ushahidi na tutawatangazia tutakapokamilisha,” alisema.

Alisema waligundua kwamba kuna maofisa utumishi na wahasibu ambao siyo waaminifu, badala yake walikuwa wakielekeza fedha kwa ndugu zao na miradi yao na wengine walishastaafu lakini bado majina yao yalikuwa yakiendelea kupokea mishahara wakati walitakiwa kuondolewa kwenye mfumo.

Alisema kwa kipindi cha Machi mosi hadi Agosti 20 mwaka huu, watumishi hewa waliogundulika ni zaidi ya 16,127 na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha. Kwa kipindi cha Agosti pekee watumishi hao hewa wangelipwa mishahara wangeisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 16.

“Uhakiki huu ni endelevu na tumegundua changamoto kubwa katika usimamizi wa mishahara ni uadilifu kwa watu waliokasimiwa madaraka. Maofisa Utumishi, Maofisa Utawala na Wahasibu wamepewa madaraka lakini wengi wao siyo waaminifu, hivyo kwa sasa tumeweka uwajibikaji kwa waajiri,” alisema.

Aidha alisema wanaufanyia mfumo wao maboresho zaidi ili uweze kuchakata taarifa nyingi zaidi ambapo pia sekta ya mishahara imeshushwa katika ngazi za chini zaidi hasa katika sekta za elimu na afya ambazo zimekutwa na watumishi hewa wengi zaidi ili waweze kuwa na taarifa za mtumishi mmoja mmoja.

Alisema upo muongozo ambao fedha za serikali zinaporejeshwa zinapitia hazina na kusisitiza kwamba wataendelea kuhakikisha wanasimamia fedha zote ambazo zilichukuliwa serikalini kinyume na utaratibu na isivyo halali zinarudishwa kwa mfumo sahihi.

Pia alisema wameongeza kasi ili kuhakikisha kunakuwa na nidhamu ya kazi na uwajibikaji kwa watumishi wa umma, hivyo wanaanda mkataba wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma na ikiwezekana utaanza kutumika mwaka ujao wa fedha.

Alisema serikali imefanya maboresho makubwa katika mishahara na motisha kwa ajili ya maslahi ya watumishi wa umma, sambamba na kuhimiza taasisi mbalimbali kuweka vitendea kazi ili kuwawezesha wafanyakazi kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Akizungumzia ajira hizo mpya Kairuki aliwatoa hofu watanzania waliokuwa wanatarajia ajira serikalini na kusisitiza kwamba walichokuwa wanasubiri ni takwimu halisi kwa taasisi ili kujua ni watumishi wangapi wameondolewa.

“Baada ya kukamilisha mchakato huo, hatua nyingine zitaendelea… Hii ni neema kwa waliomaliza vyuo, cha msingi wavute subira maana tutatoa ajira 71,496 kwa mwaka huu wa fedha na hatukuzifuta ajira. 

"Nawashauri vijana wasijiingize kwenye makundi yasiyofaa wasubiri ajira zinakuja,” alisema. 

Katika hatua nyingine, Kairuki alisema, wamepokea malalamiko zaidi ya 200 kutokana na ukiukwaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa Utumishi wa Umma ambayo inamnyima mtumishi kutotumia madaraka yake vibaya.

“Katika malalamiko hayo 142 yanahusu sheria ya maadili. Sekretarieti ya Maadili imefanya uchunguzi wa awali na malalamiko 12 yataanza kufikishwa Baraza la Maadili na hatua mbalimbali zinaweza kuchukuliwa ikiwemo kushushwa vyeo au kuachishwa kazi,” alisema.

Pia aliwaagiza maofisa utumishi kuwahudumia watumishi na kuwapa haki zao ikiwemo kuwapandisha madaraja kwa wakati pale wanapostahili. Aidha Kairuki alikemea tabia ya baadhi ya watu kughushi taarifa za utumishi wa umma na kusisitiza kwamba jambo hilo ni kosa kubwa kwa yeyote anayefanya hivyo.

“Mtu yeyote ambaye anatoa nyaraka za serikali na siyo mlengwa au anayetoa nyaraka ambayo imewekewa zuio kwa mujibu wa sheria ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Tunawasisitiza watumishi wa umma kuhakikisha wanazingatia sheria hizo na mwongozo wa utoaji nyaraka na kumbukumbu za taarifa za serikali,” alisema.

Sunday, 10 July 2016

CAMPUS VYBEZ YA TIMESFM YAKUTANISHA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUJADILI CHANGAMOTO ZA AJIRA

Watangazaji wa Kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa na Kituo cha redio cha TimesFm ya jijini Dar, Sandra Temu na Raheem wakiongoza mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm redioni ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku.

 Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  BAADHI ya wanafunzi wa elimu ya Juu kutoka katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mtangazaji wa kipindi cha Campus Vybez katika mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm radion ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku.
  Mc Pilipili akitoa kibwagizo mara baada ya kukaribishwa.
 Mc Pilipili akijitambulisha kwa vijana, pembeni yake ni Ron Fidanza, Naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde.
Msimamizi Mkuu wa radio ya TimesFm  Ron Fidanza.
 Mhadhiri wa Lugha wa Chuo cha Ualimu DUCE, Mhe. Ruben Ndimbo akijitambulisha.
 Mmoja wa waalikwa akijitambulisha.
 Meza mkuu.

Tuesday, 17 May 2016

WALIMU 35,411 KUAJIRIWA MWEZI WA 7 MWAKA HUU


Walimu 35,411 nchini wataajiriwa katika shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Watakaokaidi kwenda kuripoti katika mikoa ya pembezoni, hawataajiriwa na serikali.

Hatua hiyo imeelezwa kwamba imetokana na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu, ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa miji kwa kutegemea kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.

Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni, ikiwemo Lindi na kwingineko, lakini hawakuripoti.

Jaffo alisema ni kweli kuna walimu wengi ambao hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni. Alisema si Lindi peke yake, bali na mikoa mingine, ikiwemo Katavi na Kigoma.

Alisema kwa mwaka huu, wataajiri walimu 35,411, lakini ambaye hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini tu, hawataajiriwa tena serikalini, kama wanavyoomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi.

Wednesday, 30 December 2015

UKAGUZI WA VIBALI VYA AJIRA KWA WAGENI KUANZA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama (Mb), akifuatilia maelezo ya wajumbe wa kikosi Maalum cha kukagua vibali vya Ajira za Wageni (hawapo pichani) wakati alipokutana nao Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba, 2015, (katikati) ni Naibu Waziri (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde na Katibu Mkuu (kazi na Ajira), Eric Shitindi.
Serikali imeamua muda wowote kuanzia mwezi huu kuanza ukaguzi wa vibali vya Ajira za Wageni nchini, kufuatia muda wa siku 14 kuisha uliotolewa na serikali katika tangazo la utolewaji wa vibali vya kazi kwa wageni nchini lililotiwa saini Desemba 14, mwaka huu, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Aiira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), ambaye aliwataka waajiri wote nchini kwa muda wa siku hizo wawe wametekeleza matakwa ya Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni nchini Na. 1 ya Mwaka 2015.
“Katika taarifa tuliyoitoa mwezi huu, tuliwajulisha waajiri wote wenye waajiriwa wageni ambao wana vibali vya kazi za muda (Carry on Temporary Assignment) na wale wote wasiokuwa na vibali vya ajira vilivyotolewa na kamishna wa kazi nchini kuwa wanatenda kosa. Kamishna wa kazi amepewa mamlaka kutoa vibali vya ajira kwa wageni wanaotaka kufanya kazi nchini. Hivyo hakuna mamlaka nyingine yoyote inayoruhusiwa kutoa vibali vya ajira kwa wageni,” amesema Mhagama
Amesema hayo, Tarehe 29 Desemba, 2015, Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na kikosi maalum kitakachoendesha operasheni hiyo chenye wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uhamiaji na Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), ikiwa lengo ni kufuatilia kama agizo lililotolewa na serikali limefuatwa na kuhakikisha taratibu zinazopaswa kufuatwa katika utoaji wa vibali vya ajira zinazingatiwa.
“Serikali ilitoa muda wa siku 14 kwa waajiri wote wawe wametekeleza matakwa ya Sheria Na. 1 ya mwaka 2015 vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.” Alisitiza Mhagama.
Mwezi Machi, mwaka huu Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni nchini Na. 1 ya Mwaka 2015 (The Non-Citizens (Employment Regulation) Act)). Sheria imeanza kutumika rasmi tangu tarehe 15 Septemba, 2015. Sheria hiyo inaanzisha Mamlaka moja yautoajiwa vibali vya ajira kwa wageni na Mamlak ahiyo ni Kamishna wa Kazi.

Thursday, 23 July 2015

TOP JOBS FOR THIS WEEK

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA