MAGUFULI:NITAPUNGUZA GHARAMA ZA VIFAA VYA WENYE ULEMAVU
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa mjini Kigoma kwenye uwanja wa Kawawa katikia mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo na kuhudhuriwa na Malefu ya wananchi.
Dr. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo amesema mara atakapoingia ikulu kwa ridhaa ya watanzania na kuunda serikali, uongozi wake utaangalia njia nzuri ya kufanya ili kupunguza gharama za vifaa mbalimbali vya watu wenye ulemavu wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi Albino ili waweze kuvipata kwa urahisi na kuwarahisishia mahitaji muhimu katika maisha yao.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Kawawa mjini Kigoma.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma na mgombea ubunge jimbo la Kigoma mjini Dr. Walid Kaborou akiomba kura kwa wananchi wa Kigoma mjini.
Kada wa CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu nchini Bw. Amon Mpanju akimpiga debe mgombea urais Dr. John Pombe Magufuli.
Mzee Yusuf Makamba akihutubia wananchi katika mkutano huo.
Bendi ya TOT ikitumbuiza katika mkutano huo.
Bango hili linasema Sisi Chama cha mawese Tumeamua kura zote kwa Magufuli kwa Maslahi ya Umma.
Kundi la Orijino Kemedi likifanya vitu vyake jukwaani katika mkutano huo.
Msanii Mwigizaji Masanja Mkandamizaji akikandamiza mbele ya umati wa wananchi waliojitokezaq kwenye mkutano huo.
Msanii Ma Dee wa Tiptop Connection akipagawisha wananchi katika mkutano huo.
Ulinzi nao uliimarishwa ili kuhakikisha usalama.
Kundi la ngoma za asili likitumuiza katika mkutano huo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Mh. Peter Serukamba katika kata ya Kalinzi mkoani Kigoma.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea udiwani wa jimbo la Kigoma Kaskazini.
Wananchi wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli alipowasili katika Tarafa ya Nguruka.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wakati aliposimama kijiji cha Kazuramimba akiwa njiani kuelekea Kigoma mjini.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na wanachama wapya wa CCM waliojiunga na chama hicho kutoka vyama vya NCCR, Chadema na ACT katika mkutano uliofanyika tarafa ya Nguruka mkoni Kigoma.
Baadhi ya Kadi za vyama mbalimbali zilizorejeshwa na wanachama wa vyama hivyo na kukabidhiwa kadi za CCM.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akipokea kadi za vyama mbalimbali zilizokabidhiwa kwake kutoka vyama vya upinzani kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akikmabidhi ilani ya uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo ka Kigoma Kaskazini Mh Hasna Mwilima.
Vijana mbalimbali wakiwa juu ya paa la shule ya msingi Nguruka wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli.
Magufuli Hapa ni Kazi tu .
Wananchi wakipunga mikono yao wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia katika tarafa ya Nguruka.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma katika mkutano wake wa kampeni leo.
Kila bango ni Magufuli tu.
Hata juu ya paa tutamsikiliza tu Dr. John Pombe Magufuli
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kada wa CCM Bi Asha Baraka ambaye ni mzaliwa wa Tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwasili katika mkutano wa kampeni uliofanyika tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma leo.