Thursday, 29 May 2014

Ghasia zaidi, kupinga kombe la dunia.


140528094756 brazil worldcup 512x288 reuters nocredit 7c280

Polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu Brasilia wanaopinga kuandaliwa kwa kombe la dunia nchini humo.
Polisi walipigwa kwa mawe huku mamia ya waandamanaji wakijaribu kufika uwanja wa kitaifa ambako kombe hilo lamshindi wa kinyang'anyilo  limewekwa
Kikundi cha watu asilia wanaodai haki zao za kumiliki ardhi walijiunga na maandamano hayo
Haya ni maandamano ya hivi karibuni nchini Brazil kupinga gharama iliyotumiwa kuandaa kombe hilo.
Maafisa wakuu wanasema kuwa karibu watu 1,500 walihudhuria maandamano hayo yaliyofanyika Jumanne.
Waandamanaji hao walijaribu kwenda katika uwanja wa kitaifa ambao utakuwa mwenyeji wa mechi kadhaa za kombe la dunia ingawa polisi waliwazuia.
Polisi mmoja alijeruhiwa kwa mshale uliorushwa na mmoja wa waandamanaji wakati wa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji hao.
Waandamanaji hao walitatiza pakubwa msongamano wa magari mjini Brasilia kwa masaa kadhaa.
Mwaka jana takriban watu milioni moja walishiriki maandamano kote nchini humo kutaka huduma bora zaidi za umma na kulalamikia ufisadi na gharama ya juu iliyotumiwa kuandaa kombe la dunia
CHANZO BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA